JESHI LA POLISI KUUNDA TUME KUCHUNGUZA KIFO CHA MWANDISHI DAUD MWANGOSI, CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI IRINGA CHATOA MSIMAMO MKALI JUU YA TUKIO KWA JESHI LA POLISI IRINGA.
KAMISHNA WA OPERESHENI WA JESHI LA POLISI, PAUL CHAGONJA.
Mwandishi wa Chanel Ten marehemu, Daud Mwangosi (mwenye kamera) akiwa mwenye furaha muda tu mfupi kabla ya kumkuta umauti akimchukua picha Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, MICHAEL KAMUANDA kulia katika eneo la kijiji cha Nyololo mjini Iringa kabla ya kuanza kwa vurugu na hatimaye kufariki dunia.
KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA IRINGA, MICHAEL KAMUANDA.
JESHI la Polisi nchini limeunda tume itakayochunguza kifo cha Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel TEN, Marehemu Daud Mwangosi kilichotokea mjini Iringa wakati Jeshi la Polisi likipambana na wafuasi wa Chadema waliokuwa katika ufunguzi wa tawi la chama hicho katika Kijiji cha Nyololo mjini Iringa.
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja alisema kuwa uchunguzi huo utavishirikisha vyombo vya usalama kutoka Jeshi la Polisi pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Pakuwa Jeshi la Polisi limeunda tume itakayowahusisha Maofisa kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ pamoja Mkurugenzi wa Makosi ya Jinai Robert Manumba, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema ili kubaini ukweli kuhusu kiliochosababisha kifo cha mwandishi huyo basi tusubiri matokeo ya uchunguzi huo’ alisema Chagonja.
Marehemu Mwangosi amefariki dunia jana wakati baada ya kulipukiwa na kitu kinachachodaiwa kuwa ni bomu wakati chama cha Demokrasia na Maendelo (Chadema) kikifungua tawi la chama chake katika Kijiji cha Nyololo mjini Iringa.
No comments:
Post a Comment