Khatibu wa Swala ya Ijumaa hapa mjini Tehran amesema, ulimwengu wa kibeberu unapaswa kutambua kwamba, taifa la Iran limestahamili magumu mengi na kwamba, kwa fadhila za Mwenyezi Mungu litashinda njama na mipango yote ya maadui.
Ayatullah Ahmad Khatami amesema hayo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya Swala ya Ijumaa jijini Tehran na kubainisha kwamba, hatua ya madola ya kibeberu ya kushadidisha mashinikizo dhidi ya Iran na kutaka kuonyesha kwamba, Iran kuna mgogogoro sambamba na hatua yao ya kueneza uzushi na uongo dhidi ya taifa hilo ni baadhi ya mikakati ya maadui ya kukabiliana na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Ayatullah Khatami amewatahadharisha maadui wa mapinduzi ya Kiislamu akiwaambia kwamba, wanapaswa kutambua kwamba, hii leo taifa la Iran linahisi kuwa na nguvu na uwezo kuliko kipindi chochote kile. Ayatullah Khatami amesema, madola ya kibeberu yanataka kuonyesha kwamba, kushadidisha kwao vikwazo dhidi ya Iran kunatokana na Tehran kung'ang'ania kujipatia teknolojia ya nyuklia.
Amesema, huu ni urongo wa wazi kwani katika kipindi cha miaka 30 iliyopita madola hayo yalikuwa yakiliwekea vikwazo taifa hilo na wakati huo hakukuweko na dalili zozote za kutaka kujipatia teknolojia ya kisasa ya nishati ya nyuklia kwa matumizi ya amani.
Kutoka: irib
No comments:
Post a Comment