Halmashauri Kuu ya Taifa ya CHAMA CHA MAPINDUZI CCM iliyokaa kikao chake jana tarehe 10 November 2012, imependekeza Ndugu. Phillip Mangula kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara huku Rais wa Zanzibar Mweneyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, akipendekeza kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.
Nape Nnauye ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Kizota,amesema majina hayo yatapigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu siku ya jumanne.Hata hivyo ndugu Nape, amewaambia waandishi wa habari kuwa kikao cha NEC kimepitisha kwa kishindo jina la Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti CCM Taifa.
Pia kikao cha NEC kimefanya Mabadiliko kidogo ambapo leo wajumbe wa NEC nafasi kumi bara,na kumi Zanzibar watapigiwa kura leo tarehe 11 Novemba badala ya kesho, na matokeo yatatangazwa mara baada ya uchaguzi kumalizika.Wajumbe wote wa mkutano kutoka mikoa yote wameshawasili.
Wakati huo huo Rais Jakaya Kikwete kabla ya kufungua mkutano mkuu ataweka jiwe la msingi la Makao Makuu mapya ya CCM eneo la Makulu.
No comments:
Post a Comment