Saturday, January 5, 2013

UJIJI: Mji wa kihistoria na historia iliyotukuka

Nyumba ya Makumbusho ya Dr Livingstone iliyopo katika eneo la Ujiji mkoani Kigoma
Ujiji ustaarabu ni asili yake. Pasi inayotumia mafuta ya taa,ambapo mtumiaji hujaza upepo na kuwasha kwa kiberiti na kuanza kuitumia. Huu ni uthibitisho wa kuwa watu wa Ujiji tangu zama na zama walikuwa wanavaa mavazi mazuri na yaliyonyooshwa kwa pasi


Birika la shaba ni uthibitisho kuwa wakazi wa Ujiji ni watumia wakubwa wa kahawa na chai tangu zamani. Na makubadhi yanaonesha kuwa kwa wakazi wa Ujiji, usafi ni sehemu ya maisha yao. Katika jamii nyingi, uvaaji wa viatu hutafsiriwa kama ni sehemu ya usafi na ustaarabu wa hali ya juu
Miembe hii ilipandwa kipindi ambacho biashara ya utumwa ikiwa imeshamiri. Hii ni njia "route" walipokuwa wakipita watumwa. Miembe iliyopandwa kwa sura hii, inapatikana pia Tabora na Bagamoyo

Mnara huu ni mahali ambapo Dr David Livingstone alikuwa ameweka makazi yake ya muda wakati akiwa katika kazi yake ya kusambaza dini "ukristo" pamoja na kupambana na biashara ya watumwa iliyokuwa imeshamiri katika karne ya 19
Sanamu ikionesha siku ambapo Henry M.Stanley alikutana na Dr Livingstone baada ya safari ndefu ya kumtafuta. Inasemekana hapa, Henry M. Stanley anasema "Dr Livingstone, I presume"
Shule ya msingi KARUTA (Zamani seminari ya UJIJI) ilijengwa enzi za utawala wa wajerumani. Ilipewa jina la KARUTA kama heshima kwa Sheikh Amri Abeid Karuta, Mshairi maarufu, mzaliwa wa Ujiji aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa jimbo la Magharibi (Western Province)na pia waziri wa kwanza wa sheria katika serikali ya madaraka ya Tanganyika ya mwaka 1960

No comments: