Monday, June 3, 2013

Chuo cha Ualimu Kasulu kinachangamoto kubwa ya ufundishaji somo la IT

CHUO cha Ualimu Kasulu mkoani Kigoma kinakabiliwa na changamoto kubwa ya ufundishaji wa somo la teknolojia ya habari na mawasiliano (IT), kutokana na ukosefu ya komputa.

Akizungumza mwishoni mwa wiki chuoni hapo, mkuu wa chuo hicho Joseph Mwangamila alisema chuo hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo upungufu wa komputa za kujifunzia sambamba na darasa kwa ajili ya masomo kwa vitendo.

Akipokea msaada wa komputa sita zenye thamani ya shilingi milioni sita zilizotolewa na kampuni ya Vodacom kupitia Vodacom Foundation, mkuu huyo wa chuo alisema kutokana na upungufu wa komputa, ufundishaji wa somo hilo umekuwa mgumu chuoni hapo.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho Askofu Dkt Gerald Mpango aliiomba Vodacom kufadhili ujenzi wa jengo la darasa moja na vifaa kwa ajili ya mafunzo ya sayansi kwa vitendo. 

Aidha mkuu wa chuo hicho Mwl Joseph Mwangamila pamoja na kupongeza Vodacom kwa msaada huo alisisitiza Vodacom kuweka kipaumbele katika mipango yao kukisaidia chuo kuondokana na changamoto hizo ili kuboresha zaidi mazingira ya elimu chuoni hapo. 

Mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho Elisi Kasongo alisema kuwa dunia ya sasa inahitaji ufahamu zaidi wa teknolojia ya habari ilikwenda sambamba na mahitaji kwa wakati huu, Kupitia Kompyuta ni rahisi mwalimu kupata mada na vitu mbalimbali vya kufundishia wanafunzi jambo ambalo kukosekana kwa kompyuta hufanya funzo la somo hilo chuoni hapa kuwa gumu hivyo tunahitaji msaada zaidi” alisema mwanafunzi huyo. 

Wanafunzi wa chuo hicho wameishukuru Vodacom Tanzania kwa msaada walioutoa nakuahidi kutumia kikamilifu kwa manufaa yao na wanafunzi wajao.

Kwa mujibu wa Meneja wa Vodacom Foundation Bi. Grace Lyon msaada huo unalenga kupunguza changamoto hiyo inayofanya wanachuo kukosa fursa ya pamoja wakati wa somo hilo.

Bi. Grace alisema kuwa, iwapo Kompyuta hizo zitatumiwa vyema na kwa usahihi zitapunguza changamoto ya uhaba wa Kompyuta jambo ambalo litaongeza ufanisi katika somo hilo chuo ni hapo. 

Kompyuta hizo tano zilikabidhi wa kwa niaba ya Vodacom Foundation na mshindi wa shindano la ”Vodacom Mahela” kutoka Kigoma Bw. Valerian Kamugisha aliyeshinda shilingi milioni mia moja hivi karibuni. 


No comments: