Ndugu
zangu,
Inasemwa na wanataaluma kuwa, elimu ndio njia
ya uhakika ya kumuweka mtanzania wa kawaida kwenye daraja la kati kuliko njia
nyingine nyingi zinazofahamika. Kwa mantiki hiyo inafaa zaidi watanzania wengi
wapate elimu yenye lengo la kuwakomboa, kifikra na kiujuzi na hatimaye
waelimike kwa lengo la kuwasaidia kwa maana ya kuwatumikia wananchi wenzao
wengi.
Nilisoma moja ya makala ya ‘mentor’ wangu Maggid Mjengwa yenye kichwa ‘Tunawapitsha Watu Wetu Kwenye Njia Yenye
Matope Kwanini’? kwenye makala hiyo amemnukuu
Marehemu Mzee Jongo aliyepata kusema , Kusoma si kuufuta ujinga,bali ni
kuupunguza. Halafu akaendelea kwa kusema, kila binadamu ana ujinga wa jambo
moja au mia moja,kuwa na ujinga wa jambo si kosa. Nina ongezea kwa kusema
mwanadamu asiye jitambua na kuishi maisha kama nakala ya gazeti ana matatizo.
Je vipi kuhusu binadamu, kwanini
binadamu fulani anaishi, kwanini Fulani alizaliwa duniani? Kwa maswali hayo
kila mmoja atapata picha kuwa hakuna binadamu aliyeletwa duniani bila malengo
au madhumuni fulani, hivyo basi kila binadamu ana malengo au madhumuni fulani
ya kuishi duniani. Hakuna kiumbe chochote kilichopo duniani kisicho na
madhumuni fulani ya kipekee.
Je ni binadamu wangapi wanaishi
maisha yaongozwayo na malengo? Maisha yasiyoongozwa na malengo hayana maana
yoyote, maisha huwa na maana pale yanapoongozwa na malengo.Na binadamu yeyote
anayeishi maisha yanayoongozwa na malengo huleta tofauti kubwa katika
maisha na dunia nzima.
Tunaishi katika utamaduni
uliojaa vitu na anasa ambazo kwazo mafanikio yetu hupimwa kwa vitu
tunavyovifanya au mali tunayochuma. Kutokana na hali hii maisha yetu ya kila
siku yanakabiliwa na mambo ya kufanikisha na malengo ya kutimizwa.
Mawazo yetu wakati wote yanalenga vitendo. Ukitazama sekta zote, viwandani maofisini, mashambani, mashuleni, vyuoni na hata majumbani mwetu, msisitizo mkubwa unawekwa katika malengo na namnaya kuyafikisha malengo hayo. Lakini malengo yenyewe ni ya kupata vitu vinavyoshikika. Kwa mfano, kutengeneza bidhaa mpya, kuongeza soko la bidhaa zao n.k. Vyuoni huweka malengo ya kuanzisha program mpya, au kuongeza nafasi za hosteli, n.k. kuwasomesha watoto waliopo, kujenga nyumba, kununua gari n.k.
Mawazo yetu wakati wote yanalenga vitendo. Ukitazama sekta zote, viwandani maofisini, mashambani, mashuleni, vyuoni na hata majumbani mwetu, msisitizo mkubwa unawekwa katika malengo na namnaya kuyafikisha malengo hayo. Lakini malengo yenyewe ni ya kupata vitu vinavyoshikika. Kwa mfano, kutengeneza bidhaa mpya, kuongeza soko la bidhaa zao n.k. Vyuoni huweka malengo ya kuanzisha program mpya, au kuongeza nafasi za hosteli, n.k. kuwasomesha watoto waliopo, kujenga nyumba, kununua gari n.k.
Hata hivyo, watu hupishana
katika malengo. Baadhi ya watu wanaamini kufanikiwa ni kuchuma au kulimbikiza
mali. Wengine kwao kufanikiwa ni kupata watoto, wengine kusoma hadi kupata
digrii ya Chuo Kikuu, wengine kufanikiwa ni kuokoka,na wengine mafanikio ni
kuhama kutoka kanisa moja kwenda jingine wengine ni kujiunga na mtandao wa
kijamii kama ‘face Book,wengine mafanikio ni kula nyama kila siku n.k.
Mshauri namba moja wa mambo
ya kijamii na mafanikio, Kopmeyer, katika kitabu chake ‘Thoughts To Build On’,na
‘Here Is Help’ anasema, mafanikio
yanaanza na mambo matatu. Kwanza, Lazima mtu awe na utashi utakaomfanya aamini kwamba nayeye
anaweza kufanikwa. Hamasa hii ndiyo
chachu ambayo hufananishwa na roketi iendayo mwezini, yaani lengo
analokusudia.
Pili, Lazima mtu awe na
hamasa ya kutafuta taarifa anazohitaji kujua na kuzifanyia kazi ili aweze
kujihakikishia mafanikio. Lakini shughuli yoyote ile hata iwe inahamasisha
kiasi gani inaweza kuwa na matokeo mazuri au mabaya. Kwa hiyo, kabla mtu
hajakurupuka na kuanza kukimbia kuelekea upande usiofaa, Lazima ahakikishe Nia
na utashi wake umemhamasisha yeye kwa
kiasi cha kutosha cha kumfanya awe tayati kulipa gharama ya mafanikio yake ili
kufikia malengo aliyojiwekea kabla ya kuanza kufanya lolote. Lazima kuwepo na lengo - na lengo lenyewe Lazima liwe
limeamuliwa kabla ya kuanza hatua za kulifikia. Vinginevyo atakuwa amekusanya
taarifa ambazo hatazitumia baadaye.
Kila unachokitaka katika
maisha kina gharama yake. Gharama hii siyo Lazima
iwe katika fedha. Ingawa wakatiwote fedha zinaweza kuhusika. Ni gharama
nyingine zinazohitaji ili kuleta mafanikio ndiyo unapaswa kuwa tayari kuzibeba.
Gharama hizi ni pamoja na kuwa tayari kujitolea muhanga wewe binafsi katika
muda wako, juhudi zako, katika kujifunza, katika kupanga mambo yako, kutafuta
ufumbuzi na kufanya yale yanayopaswa kufanywa na katika wakati unaopaswa
kufanya. kama anavyodai Komeyer, mara nyingi elimu ya madarasani hushindwa kutoa
hamasa ya aina hii.
Juzi,nilipokuwa
Mjini Mbeya,
nimekutana na mwanafunzi wa kidato cha sita,alipata kusoma makala zangu
siku za
nyuma. Kwa muda wake wa ziada analima bustani ya mboga nyumbani kwao
kila
atokapo shule, hutumia nusu saa kujishughulisha na bustani
yake,anatambua umhimu wa muda, anafahamu kwamba bila yeye hakuna mjomba
wala mfadhili atakaye mkomboa. Ameweka lengo
la kuwa mjasiriamali mwenye malengo, kwa kipindi cha miaka mitano ijayo
anategemea kufanya maajabu katika dunia ya wajasiriamali.
Tatu, pamoja nayo kuna jambo jingine muhimu, nalo linahusu fomyula
ya mafanikio. Lazima mtu awe na fomyula rahisi ya kumuwezesha kufikia malengo
yake.
Tanzania, na nchi nyingine za dunia ya tatu kama hii ya kwetu, kuna taasisi nyingi za
kifedha ambazo zinasaidia watu wenye kipato cha chini kwa kuwapatia mikopo, lakini
wengi wa wanaokopeshwa bado hawana elimu ya utambuzi na wengi wao hawana
malengo,hawafahamu tofauti iliyopo kati ya mikopo mizuri na mikopo hatari (good
debit and bad debit). Baadhi ya wanaopewa mikopo wananunua nguo na wengine
wananunua vifaa vya ndani,na wengine wanaenda mbali na kununu simu,na orodha ni
ndefu hapa.
Lakini tujiulize: (1) Je, watu
hawa wanaokusudiwa wana nia ya kutosha kuwashawishi kwamba umasikini ni mbaya
na ni Lazima waondokane nao? (2) Je, watu hawa wamehamasishwa vya kutosha kiasi
cha wao kuamini kwamba wanaweza kupambana na umasikini na kuuondoa wao wenyewe,
na kwamba kazi ya serikali au wafadhili ni kuwaunga mkono tu, lakini wao
wenyewe ndiyo wanatakiwa kuwa washiriki wakuu? (3) Je, watu hawa wanao ujuzi au
stadi zitakazowasaidia kufanya yale wanayotaka kuyafanya ili kuondokana na
umasikini?
Ni dhahili mipango yoyote
yenye lengo la kumkomboa mwananchi, kama
vile MKUKUTA, haiwezi kufanikiwa endapo mambo haya matatu hayatazingatiwa
ipasavyo. Mitaji ya fedha peke yake, haiwezi kuwaletea mafanikio walengwa
bila kuwepo kwamba mambo haya ambayo kwa
mtazamo wangu ni mhimu walengwa wa mikopo na misaada hiyo wakipewa elimu ya
kujitambua na kujiamini.
Kwa mafano, kama mtu
anadhani au anaamini, kutokana na sababu yoyote ile, kama vile kulogwa au Mungu
ndiyo alivyompangia kwamba umasikini ndiyo stahili yake, huwezi kumsaidia mtu
huyu kuondokana na umasikini. Ukimpa mtaji wa fedha atakula na kubaki maskini.
Kama mtu anaukataa umasikini lakini hayuko tayari kujituma kufanya kazi kwa
bidii, naye huwezi kumsaidia. Kama mtu anaukataa umaskini, na yuko tayari
kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii, lakini hana ujuzi au stadi wa kufanya
anachokusudia kuondoakna na umasikini, pia mtu huyu hawezi kuondokana na
umasikini huo.
Tutabuni miradi mingi,yapo
mashirika mengi yasiyokuwa ya kiserkali (NGO), tutabuni sera za kila aina zenye
ubora usiyo na kasoro hata moja,tutaanzisha vyuo vikuu kila mkoa na kila wilaya na kila kata, na kozi
za kila aina na wanafunzi watapewa mikopo (madeni) lakini bila elimu ya
kujitambua na kujifahamu ni kazi bure, ni kutaka kuvuka bahari ya Hindi kwa
mtumbwi uliotoboka. Tunao wanafunzi wengi waliohitimu vyuo vikuu miaka nenda
rudi hawana kazi, hawana cha kufanya,wamekuwa mzigo kwa taifa na kwa familia,wengi
wao wamekuwa washabiki wa siasa za bongo.Wengine wanajivua magamba na wengine
wana vaa magwanda.Ili mradi kunakucha.
Ndiyo- Binadamu aliyeamua kupata kitu fulani
maishani hajui sababu za kushindwa na wala hana sababu zinazoweza kumzuia.
Utafiti uliofanywa na Jenny
Fulbright, ‘10 Secrets on Successful Entrepreneurship’ anasema mafanikio yapo kwa ajili ya mtu
yoyote, lakini ili mtu afanikiwe Lazima
ajue au azingatie mambo 10 yafuatayo... (Itaendelea
Jumatatu Ijayo)
No comments:
Post a Comment