Saturday, October 13, 2012

Amiri jeshi mkuu: Wairan si wachokozi ila hatutafumbia macho uchokozi wa aina yeyote

Ayatollah Ali Khamenei ameyasema hayo alipokuwa akikagua gwaride la majeshi ya ulinzi ya Jamhuri ya kiislam ya Iran akiongozana sanjari na majenerali na wakuu wengine wa jeshi hilo. Ayatollah Ali Khamenei aliongeza kwa kusema:Jamhuri ya kiislam ya Iran si wachokozi ila jeshi letu halitafumbia macho aina yeyote ya uchokozi utakao fanywa dhidi ya Iran Pia aliwatahadharisha maadui wa Iran kuwa: wasithubutu hata kufikiria kuishambulia Iran kijeshi kwani matokeo yake yatakuwa ni madhara makubwa kwao.

ABNA.co

No comments: