Sunday, May 12, 2013

Dk. Hoseah: Mimi ni mpambanaji


Dk. Hoseah alitoa kauli hiyo mwanzoni mwa wiki hii alipokuwa akizungumza katika kipindi cha ‘Dakika 45’ kinachorushwa hewani na kituo cha Televisheni cha ITV alipoulizwa kuwa haoni kauli yake aliyoitoa hivi karibuni wakati akizungumza na wakuu wa madhehebu ya dini kuwa rushwa ni janga la kitaifa inaonyesha kuwa ameshindwa kazi. 

“La hasha, siwezi kusalimu amri kwa sababu mimi ni mpiganaji nawe unafahamu. Nilisema rushwa ni janga la kitaifa kwa kwa sababu kubwa tatu; kwanza haibishaniwi kuwa rushwa bado ni kero, kero kwa wananchi wa kawaida, kero kwa maana ya taifa, kero kwa maana bado ni tatizo na hivyo kuna haja kabisa ya kuongeza bidii zaidi kuliko bidii zilizopo ili kuifanya rushwa iweze kushughulikiwa ipasavyo,” alisema Dk. Hoseah. 

Alisema pia kumekuwepo na majanga mengine nchini, akatolea mfano janga la ukimwi na kwamba taifa limeweka msisitizo mkubwa kwenye kampeni, uwezeshwaji na wananchi kushirikishwa na kuamka hivyo kwa mantiki hiyo alidhani katika mtazamo wake kwamba rushwa ikifanywa kwa mrengo wa namna hiyo (janga la kitaifa) anafikiri itapungua kwa kiasi kikubwa kuliko ikaachiwa TAKUKURU peke yake kana kwamba ni tatizo lake pekee. 

“Janga la taifa ni kama mnavyoona ukimwi, kila mtu sasa ashiriki, kila mtu aogope kutoa rushwa, tatu; ili kutatua tatizo ambalo ni janga lazima wananchi na jamii washirikishwe na ndiyo maana utatambua kuwa nilizungumza haya wakati naongea na wakuu wa madhehebu ya dini na wamenielewa sana na hasa nilipotamka kuwa ni janga la taifa,” alisema Dk. Hoseah. 

Alieleza kuwa viongozi hao wa dini wamekubali kuchukua sehemu yao ya kuhakikisha kwamba wanawahubiri waumini wao kwamba rushwa ni dhambi na namna gani ya kuachana kabisa na rushwa.

Pamoja na mambo mengine, alisema Tanzania ni nchi na Mwenyezi Mungu ameibariki hivyo Watanzania wanapaswa kutambua hiyo kwamba nchi yao ni kubwa yenye misitu, hali ya hewa nzuri, maziwa makubwa hivyo wasijisahau wakaliacha tatizo la rushwa likatawala maisha yao yote.

Kigoma yazidi kupendeza

Mandhari ya stendi mpya ya daladala stesheni mjini Kigoma

Saturday, May 11, 2013

Muonekano wa jiji la Dar ukiwa angani

Chanzo: www.wavuti.com

WACHINA KWA VITUKO: PICHA ZA JENGO LINALOFANANA NA UUME ZATOLEWA NA GAZETI LA CHAMA TAWALA NCHINI CHINA!!!


Gazeti la chama tawala cha china, People’s Daily ambalo limezoea kuwa kitovu cha kusambaza habari, sasa limejikuta likiwa habari baada ya watu wenye fikra za kitukutu kuona jengo jipya la gazeti hilo limefanana na nyeti za kiume.
 
Jengo hilo lenye urefu wa mita 150, hivi sasa bado linaendelea kujengwa jijini Beijing. Kutokana na muundo huo usiokua wa kawaida, picha za kibunifu zikaanza kuibuka katika website ambayo ni kama “Twitter ya China,” inayoitwa Sina Weibo.


Kwa sasa Wachina wakitafuta jengo hilo, wanakutana na ujumbe“kuendana na sheria, kanuni na sera husika, matokeo ya utafutaji wako (search results) hayawezi kuonyeshwa."
 
Mwandishi wa Reuters, Anita Li amesema “hii inaonyesha frustrations miongoni mwa vijana watumiaji wa internet nchini China, na pia inaonyesha ni kiasi gani “wakubwa” wako sensitive kwa hata vitu vidogo vya kipuuzi online.”

Upambaji wa harusi zetu Kigoma

Maandalizi ya sherehe ya harusi katika ukumbi wa Kibo Peak mjini Kigoma

Friday, May 10, 2013

Syria ipo tayari kujibu mapigo ya Israel

Syria imetishia kujibu mashambulio yoyote mapya kutoka Israel huku washirika wake wanamgambo wa Hezbolla wakisema Syria itawapa silaha zitakazobadili kile walichokitaja kuwa silaha za kubadilisha hali ya mambo.

Naibu waziri wa mambo ya nje Faisal Muqdad amesema maagizo yametolewa ya kukabiliana mara moja na shambulio lolote jipya kutoka Israel. 

Duru kadhaa za Israel zimesema mashambulio ya Ijumma na Jumapili wiki iliyopita yalilenga shehena ya silaha zilizokuwa zikipelekwa kwa kundi la Hezbollah la nchini Lebanon lakini Muqdad amekanusha madai hayo. 

Syria Kerry na Lavrov wazungumzia Syria Syria imeukaribisha mpango wa pamoja wa Marekani na Urusi wa kutafuta suluhisho la kisiasa ili kumaliza vita vya miaka miwili lakini wakati huo huo imeshutumu sharti la Marekani la kumtaka Rais Bashar al Assad kujiuzulu. 

Assad yuko tayari kwa wachunguzi 
Serikali ya rais Assad imesema pia iko tayari kupokea kundi la Umoja wa Mataifa kuchunguza madai ya kutumika kwa silaha za kemikali nchini humo. 

Na mjini Beirut,kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah amesema Syria italipa kundi lake silaha alizozitaja kuwa zitakazobadili mkondo wa mambo yalivyo sasa na kukabiliana na Israel kutoka eneo la milima la Golan. 

Israel ilinyakua eneo hilo la Golan kutoka kwa Syria katika vita vilivyodumu kwa siku sita mwaka 1967. Israel imekuwa ikionya mara kwa mara kuwa itaingilia kati kuzuia kupewa kwa wanamgambo wa Hezbollah silaha. Hezbollah inashirikiana na majeshi ya Assad katika maeneo kadhaa nchini Syria.

Utawala wa Assad unategemea pakubwa usaidizi wa wanamgambo hao na gazeti moja la Lebanon Al Akhbar limemnukuu Assad akisema kuwa Syria italipa kundi hilo chochote kwa uaminifu wake. 

Monday, May 6, 2013

Kauli ya BAKWATA kuhusu mlipuko uliotokea Kanisani Olasiti, Arusha

MK/HB.VOL.6/013/1 

06/05/2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI    

TAMKO LA BARAZA KUU LA WAISLAMU WA TANZANIA BAKWATA JUU YA MLIPUKO WA BOMU - ARUSHA

Assalaam alaykum warahmatullahi wabarakaatuh.
Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania BAKWATA, limepokea kwa masikitiko makubwa tukio la kurushwa bomu Kanisani na kusababisha upotevu wa maisha na majeraha kwa watu wengi wakati wa sherehe ya uzinduzi wa jengo la Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Orasiti, Arusha.

Kimsingi hili ni jambo la kusikitisha, kukera na kufadhaisha sana kutokea hapa nchini. Watanzania kwa miaka mingi, tumezoea hali ya utulivu na amani na tukio kama hili ni changamoto kwa usalama wa Watanzania wote nchi nzima Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania BAKWATA linalaani kitendo hicho cha kikatili na inaviomba vyombo vya dola kufanya jitihada zote kuhakikisha wahusika wanakamatwa na wanachukuliwa hatua, kwani msiba huu ni wetu sote, Wakristo na Watanzania wote.

Kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania mimi Sheikh Issa Bin Shaaban Simba Mufti wa Tanzania nawapa pole wafiwa wote katika tukio hilo na kuwaombea dua majeruhi na Mwenyezi Mungu (SW) awape tahfif na wapone haraka na kurudi katika shughuli zao za kila siku.
Wabillahi Tawfiiq.

SHEIKH ISSA BIN SHAABAN SIMBA.
MUFTI NA SHEIKH MKUU WA TANZANIA BARA.

Saturday, May 4, 2013

Ubunifu na Vipaji

Watoto hawa walikutwa na mdau wa blog hii wakiwa wanakusanya udongo kwa ajili ya kutengenezea magari. Vipaji kama hivi vikiendelezwa ni hazina kwa taifa letu

Israeli regime has attacked Syria: US officials


Two US officials say the Israeli regime has “most likely” conducted an airstrike on Syria, as the Syrian army continues to regain control of militant-infested areas. 

US media quoted the unnamed officials as saying that Tel Aviv most likely carried out the attack "in the Thursday-Friday time frame," claiming, however, that the regime’s fighter jets “did not enter Syrian airspace.” CBS News cited US sources as saying the Israeli warplanes targeted “a warehouse.” 

There has been no official confirmation from Syria or any comments from the Israeli regime. Syrian Ambassador to the UN Bashar Ja'afari said that he is “not aware of any attack right now." The Pentagon also declined to comment on the issue. 

The CNN news channel also reported that the Pentagon had collected information showing Israeli warplanes overflying Lebanon during the time frame of the strike. In January this year, Israeli warplanes also targeted a research facility on Syrian soil. 

Meanwhile, the Syrian army is continuing to advance in the Al-Qusayr region near the border with Lebanon, regaining control over the town of Jousyeh. The army has also taken back the two strategic checkpoints of Arba'at Ashar and Tall Al-Hansh. 

The checkpoints overlook the eastern villages in the Al-Qusayr countryside and Lebanon's Masharih al-Qaa. The regained region is of strategic importance because there are tunnels and passageways there used by the foreign-backed militants to enter Syria and transfer arms into the country from Lebanon. 

Large numbers of foreign-backed insurgents have reportedly been killed and many others injured in the clashes with the army.

Friday, May 3, 2013

Huu ni Ujasiri wa kijinga


Tarehe 23 mwezi aprili mwaka huu majira ya saa mbili usiku nilipokea ujumbe wa maandishi katika simu yangu kutoka kwa jamaa yangu mmoja akinishtua niangalie habari katika chaneli ya ITV. Wakati huo mimi nilikuwa naangalia katika chaneli nyingine. Bahati mbaya sikuweza kukiona kipande cha habari hiyo.

Hamadi!! Nilifanikiwa kuiona habari hiyo, ingawa nilichokiona sikuamini macho yangu. Nilidhani naota. Siku ya pili yake ilinibidi niingie katika youtube ili kuthibitisha kile nilichokiona kama ni kweli au zilikuwa ni ndoto.

Habari niliyoiona iliniumiza sana kana kwamba ni mimi ndiyo nilitendewa kitendo kile. Nilishuhudia kijana mmoja anayeonekana kuwa na akili timamu kabisa akimkunja askari wa usalama barabarani aliyekuwa akitimiza wajibu wake na kumnyang’anya ufunguo wa gari.

Kitendo kilichofanywa na kijana Yule ambaye sijui nimuite kwa sifa ipi ili imfae ni cha udhalilishaji wa hali ya juu kwa binadamu na kwa jeshi la polisi kwa ujumla wake. Nilitafakari na sikupata jibu. Ni nani asiyejua umuhimu na unyeti wa jeshi la polisi katika uhai wa jamii yoyote ile. Ni nani anayeweza kushabikia pindi anapoona jeshi la polisi linagaragazwa?

Katika siku za hivi karibuni vitendo vya kuwadhalilisha polisi na jeshi la polisi vimekuwa vikiongezeka sana. Miaka michache iliyopita, mfanyakazi katika ubalozi wa nchi moja ya Ulaya alifikia hatua ya kumtemea mate askari wa usalama wa barabarani kwa kuwa tu askari huyo alimsimamisha baada ya raia huyo wa kigeni kwenda kinyume na sheria zinazoongoza matumizi ya barabara. Si hayo tu, bali pia mwaka 2010 tulishuhudia mgombea mmoja wa ubunge akimkata mtama mkuu wa polisi wa wilaya moja katika moja za wilaya hapa nchini.

Ni vigumu sana kupita mwezi mmoja kama hujasikia askari wa polisi ameshambuliwa na watu wakati akitimiza wajibu wake. Wapo wanaouawa na mbaya zaidi wananchi wanathubutu hata kuvamia vituo vya polisi na kuvichoma moto. 

Tumeshuhudia kuchomwa moto kwa kituo cha Hedaru ambapo mali na nyaraka za serikali ziliteketezwa, lakini pia tumeshuhudia mauaji ya askari wakiwa wanatekeleza kazi zao. Wananchi pia walimuua askari mkoani Tabora mwaka 2011 wakati akiwa katika operesheni ya kuteketeza mashamba ya Bangi. 

Huwa najiuliza, je ujasiri huu wa raia katika kuwadhalilisha polisi, unatoka wapi? Inakuwaje kila anayesaka umaarufu mbele ya watu basi hakuna pa kuupatia zaidi ya polisi? Ukienda katika mikutano ya wanasiasa, ni vigumu kukuta mkutano umemalizika bila kuwatupia madongo polisi. Wasanii hasa wa vichekesho (comedians) huwa hawaamini kama kazi yao imekamilika kama hawataweka kejeli kwa jeshi la polisi.

Udhalilishaji huu kwa sasa unachupa mipaka hadi sasa vibaka nao, wanadhani wanaweza kuwachezea polisi.
Tunaweza kutafakari kwa pamoja. Kama inatokea mtu mwenye akili timamu anaweza kumdhalilisha askari mwenye sare kwa kumkunja mchana kweupe mbele ya kadamnasi, atashindwa vipi kumpiga na hata kumchania sare au kumnyang’anya silaha pale atakapokutana nae vichochoroni?

Lakini pia, tunaweza kujiuliza! Kama anaweza kumkunja polisi namna ile, je ikitokea amekasirishwa na raia mwenzake atampa adhabu gani?

Cha ajabu ni kuwa, watu hawa wanaolidhalilisha jeshi la polisi, wanashindwa kufahamu kuwa ujasiri wote walionao unatokana na kazi nzuri inayofanywa na jeshi la polisi katika kuhakikisha kunakuwepo na amani na usalama katika nchi yetu.

Watu hawa wanadhani vitendo wanavyovifanya kwa askari wetu labda vitawajengea woga katika kutimiza majukumu yao. Wanasahau kuwa hizo ni changamoto katika kazi na kwamba vitendo hivyo ndo vinajenga na kuamsha ari ya askari katika kupambana na uhalifu wa aina yoyote katika jamii yetu.

Wanasahau kuwa kama usalama usingekuwepo, inawezekana hata huo muda wanaoutumia katika kuwadhalilisha askari na jeshi zima la polisi wasingeupata.

Baadhi yetu wananchi hatuelewi dhana ya polisi jamii na pia dhana nzima ya Utii wa sheria bila Shuruti. Tunadhani, Utii wa Sheria bila Shuruti kunatokana na polisi kushindwa kutumia maguvu. Uhuru tunaopewa na jeshi la polisi tunautafsiri kama uoga na kushindwa kutimiza majukumu kwa jeshi hilo. 

Tunasahau kuwa lengo la utii wa sheria za nchi bila shuruti ni kupunguza uhalifu na matumizi ya shuruti katika usimamizi ya utiifu wa sheria za nchi. Lakini pia utaratibu huu pia unasaidia kupunguza gharama katika oparesheni za kupambana na uhalifu.

Watu hawa wanapendelea jeshi la polisi linalotumia maguvu kama polisi wa kikoloni, ambapo polisi na raia walikuwa na mahusiano ya kiuadui. Raia alipokuwa akimuona polisi hata kama hana kosa, alikuwa akitimua mbio.

Askari naye ni binadamu. Anatakiwa apewe haki zake zote na heshima yake kama binaadamu. Kumdhalilisha askari ni kuidhalilisha serikali.

Binafsi nimekuwa nikifuatilia sana ripoti za kituo cha Sheria na haki za binaadamu (LHRC). Katika taarifa zake za haki za binaadamu, sijawahi kukuta mahali walipoelezea ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu unaofanywa na wananchi wakora kwa askari wetu. Swali za kujiuliza ni hili! Je, hawaoni ukiukwaji wa haki dhidi ya polisi? Au wanaona lakini wanafumbia macho ili polisi wachukue hatua katika kujihami na wao wapate cha kusema?

Wanaharakati ambao ninaamini kwa sauti waliyonayo wanaweza kukemea utovu wa nidhamu unaofanywa na raia dhidi ya askari. Watumie nafasi waliyonayo katika jamii katika kuhakikisha kuwa wananchi, wanaheshimu sheria kwa kuwaacha askari na watumishi wengine wafanye kazi zao walizokabidhiwa na umma.

Nimalizie makala haya kwa kuwaomba askari wasifadhaike kwa matukio yanayofanywa na raia wachache wasiothamini kazi nzuri ya polisi. Raia wema tupo nyuma yenu na tunathamini na kutambua kazi zenu.

Endeleeni katika kuilinda nchi yetu. Zidisheni mapambano dhidi ya wahalifu popote pale walipo bila woga wala huruma. Pia niwapongeze askari wetu kwa uvumilivu mkubwa walionao, hii ni ishara kuwa wamefunzwa na wameiva. Na kwamba wapo tayari kukabiliana na changamoto yoyote inayojitokeza kwao kwa sura yoyote ile.

Friday, April 26, 2013

Miaka 49 ya Muungano wetu

TAKUKURU haijapewa ‘meno ya kuwatafuta mafisadi papa’ - Dk HOSEA

  Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) Dkt. Edward Hosea amewataka watanzania kutoilaumu Taasisi yake katika kushughulikia rushwa ambavyo mara kadhaa zimetajwa kuwahusisha vigogo wa Serikali na wenye uwezo.

Akizungumza katika semina ya kuwaelimsha viongozi wa dini iliyofanyika jana mjini Moshi mkoani Kilimanjaro Dkt Hosea amesema Watanzania wamekuwa wakitupia na kuinyooshea kidole cha lawama taasisi yake kwa kushindwa kufuatilia kwa kina wale wanaoitwa “mafisadi papa” nchini. 

Dkt. Hosea amesema Watanzania wanasema kwa kuwa vigogo wanaotajwa na rushwa nchini wapo katika Serikali ambayo ina mamlaka na TAKUKURU, hivyo taasisi hiyo imekuwa ikiwapendelea vigogo watuhumiwa. 

Pia amesema Watanzania walio wengi ni wavivu wa kusoma sheria mbalimbali ambazo wakati mwingine zimeeleza majukumu na uwajibikaji wa taasisi husika. 

Hata hivyo, Mkurugenzi huyo amesema sio kwamba TAKUKURU imeshindwa kufuatilia nyendo za wabadhirifu wa mali za umma ipasavyo hususani wale wanaotajwa kama “Mafisadi papa” isipokuwa taasisi anayoiongoza imewekewa mipaka ya ufanyaji kazi wake. 

Aidha, amesema mara zote amekuwa akiitaka Serikali kufanyia marekebisho ya baadhi ya sheria za kuzuia na kupambana na rushwa kutokana na ukweli kwamba TAKUKURU haijapewa meno ya kuwashughulikia wabadhilifu wakubwa. 

Dkt Hosea amesema sheria zilizopo zinamtaka ashughulikie na matendo ya kati na ya chini na sio ya juu kama ambavyo wengi wanafikiri na kuongeza kuwa haina sababu ya kuilaumu TAKUKURU kwa kushindwa kuwakamata wala rushwa wakubwa. 

Semina hiyo iliwakusanya viongozi wa dini wa Kaskazini-Mashariki kwa malengo ya kuendelza juhudi za kuielimisha jamii kuhusu masuala ya rushwa na athari zake kwa jamii. 

 Source: http://www.wavuti.com

Thursday, April 25, 2013

KIGOMA: Tunashukuru

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya akizungumza na timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Taasisi ya Mifupa (MOI) mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kuhudumia mamia ya wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa ya MaweniMkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno akitoa neno la shukrani kwa kazi kubwa iliyofanywa na madaktari hao mpango ambao unatekelezwa na NHIF (Kutoka kulia kwake ni Dk. Vence wa MOI, Dk. Kisenge na Dk. Makia wa Muhimbili.;
BAADHI ya wagonjwa waliopata fursa ya kuhudumiwa na madakri bingwa katika Hospitali ya Mkoa ya Maweni mkoani Kigoma, wameushukuru Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kuanzisha mpango huo kwa kuwa umesaidia kuokoa maisha yao.

Wamesema wamefarijika sana kutokana na ukweli kwamba ni vigumu kwao kumudu gharama za kuwafuata wataalam hao katika Hospitali za Rufaa Bugando, KCMC au Hospitali ya Taifa ya Muhimbili hivyo wameiomba Serikali kupitia Mfuko huo kukarisha mpango huo ambao unasaidia wananchi hasa wa kipato cha chini.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mkoani humo baadhi ya wagonjwa walionufaika na huduma hiyo wamesema kuwa bado  wana mahitaji makubwa ya huduma ya madaktari bingwa kwa kuwa hazipatikani katika hospitali hiyo.

“Wananchi wengi wanahitaji huduma hii kutokana na urahisi wa kuwapata madaktari  hawa…ni ngumu sana kwetu kumudu gharama za kuwafuata huko waliko kutokana na hali za vipato lakini pia miundombinu ya mkoa wetu, hivyo mimi binafsi naushukuru sana Mfuko kwa kazi hii kubwa,” alisema Mkazi wa Mwanga mjini Kigoma,Zawadi Daudi.

Alisema kuwa alibahatika kupata huduma ya upasuaji kutoka kwa madaktari bingwa hao, kutokana na uvimbe wa tumbo, uliokua ukimsumbua kwa muda mrefu.

Mgonjwa mwingine Anna Sebastian alisema anamshukuru Mungu tatizo lake la tumbo, limepatiwa matibabu kwa kufanyiwa upasuaji na mabingwa hao.

Lakini, alisema ana ndugu zake wengi ambao walihitaji huduma za madaktari hao, lakini hawakuipata kutokana na muda waliokuwa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya alitoa shukrani kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kubuni mpango huo, ambao unatoa unafuu mkubwa kwa wananchi  kupata huduma za madaktari bingwa.

Alisema hayo alipozungumza na madaktari hao, ambao walifika ofisini kwake kutoa taarifa ya kuhitimisha awamu  ya kwanza ya mpango huo mkoani kwake.

Machibya alisema kumekuwa na upungufu mkubwa wa madaktari hao nchini na hasa kwa mkoa wa Kigoma hivyo kuja kwa madaktari hao,kumepunguza tatizo la wananchi kupata huduma za madaktari bingwa.

Akitoa takwimu hizo Mkurugenzi wa tiba na masuala ya kiufundi wa mfuko wa taifa wa bima ya afya(NHIF), Frank Lekey amesema  jumla ya watu 754 mkoani Kigoma, walionana na madaktari bingwa na kupata ushauri mbalimbali.

Alisema jumla ya wagonjwa 37 walifanyiwa upasuaji mkubwa,ikiwemo kufanyiwa upasuaji wa magojwa ya tumbo kwa akina mama ,magonjwa ya moyo na figo na magonjwa ya kawaida.
Alisema baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza, Mfuko utaendelea  kuratibu upatikanaji wa huduma ya madaktari bingwa kila baada ya miezi mitatu.

Alisema katika awamu hiyo ya kwanza wamebaini kuwa kuna mahitaji makubwa ya huduma hiyo ya madaktari bingwa kwa mikoa ya pembezoni mwa nchi.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umekuwa ukiboresha huduma zake mara kwa mara na kwa sasa unatekeleza mpango wake wa kusogeza huduma karibu na wanachama wake lakini pia wananchi kwa ujumla.

Kikao cha Baraza la Madiwani Biharamulo leo

Tuesday, April 23, 2013

TASWIRA YA MKUTANO WA CHADEMA MKOANI IRINGA LEO

umati mkubwa  wa  wananchi  waliofika  kusikiliza mkutano  wa Chadema  Leo Iringa mjini
katibu  mkuu  wa Chadema Dkt Slaa (kushoto) akiwa na mbunge wa jimbo la Ubungo Jonh Mnyika katika mkutano wa  wabunge wa chadema waliofukuzwa  bungeni leo katika  uwanja  wa Mwembetogwa mjini Iringa

Picha kwa hisani ya mjengwa blog




Rais Kikwete akutana na Viongozi wa Madhehebu ya Kikristo leo Ikulu

Mji mdogo wa Nguruka: Umewahi kufika hapa

Mojawapo ya karakana nyingi zinazotengeneza samani za kisasa kabisa zilizopo katika mji mdogo wa Nguruka wilayani UvinzaMoja ya mitaa ya Nguruka

Thursday, April 18, 2013

Usafiri kipindi cha mvua mkoani Kigoma



Basi la saratoga linalofanya safari ya kigoma to bukoba likiwa limenasa ktk tope kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Hapa ni kilomita chache kutoka kasulu mjini

Thursday, April 11, 2013

Taarifa ya Polisi: Tukio la mauaji ya mfanyabiahsara wa madini kwa risasi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA OFISI YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA

TUKIO LA MAUAJI

MNAMO TAREHE 09/04/2013 MUDA WA SAA 2:30 USIKU HUKO LEMARA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA, MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA JUMA S/O RASHID (45) MFANYABIASHARA WA MADINI NA NI MKAZI WA SOMBETINI, ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI KIFUANI NA MTU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GEORGE KARAU MARRIE (38) MFANYABIASHARA NA NI MKAZI WA LEMARA.

UCHUNGUZI WA AWALI ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI MKOANI HAPA ULIBAINI KWAMBA, MAREHEMU JUMA S/O RASHID, FRANCIS S/O EDWARD (37) NA MTUHUMIWA GEORGE KARAU MARRIE WALIKUWA NI WASHIRIKI KATIKA BIASHARA YA MADINI YA TANZANITE.

INASEMEKANA KWAMBA BAADAE WALIINGIA MAKUBALIANO AMBAPO MTUHUMIWA ALIKABIDHIWA MADINI AMBAYE THAMANI YAKE BADO HAIJAJULIKANA NA FRANCIS S/O EDWARD PAMOJA NA MAREHEMU ILI AKAUZE.

JUZI TAREHE 08/04/2013 MTUHUMIWA GEORGE S/O KARAU MARRIE ALIWASILIANA NA MAREHEMU PAMOJA NA FRANCIS S/O EDWARD NA KUWAAHIDI KUWALIPA FEDHA ZAO SIKU YA TAREHE 09/04/2013.

TAREHE 09/04/2013 MUDA WA SAA 2:15 USIKU, MAREHEMU PAMOJA NA MWENZAKE FRANCIS S/O EDWARD MWASHUYA WAKIWA NA GARI AINA YA HONDA LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 230 CBE WALITOKA MAENEO YA MJINI NA KUELEKEA MAENEO YA LEMARA. WALIPOKUWA NJIANI WALIKUTANA  NA MTUHUMIWA AMBAYE ALIPANDA GARI HILO HILO NA KUKAA KITI CHA NYUMA NA MAREHEMU ALIKUWA ANAENDESHA GARI HUKU MWENZAKE AKIWA AMEKAA KITI CHA MBELE CHA UPANDE WA KUSHOTO. WOTE WALIKUWA WANAELEKEA LEMARA NYUMBANI KWA MTUHUMIWA ILI AKAWAPATIE FEDHA AMBAZO ALIKUWA ANADAIWA.

WALIPOFIKA ENEO LA TUKIO, MTUHUMIWA ALIAMURU GARI HILO LISIMAME NA KISHA AKATOA BASTOLA NA KUMPIGA MAREHEMU SEHEMU YA KIFUANI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO NA KISHA KUMJERUHI KWA RISASI FRANCIS S/O EDWARD MWASHUYA SEHEMU YA KICHWANI.

MARA BAADA YA MAUAJI HAYO, MTUHUMIWA ALIMPORA  FRANSCIS S/O EDWARD FEDHA TASLIMU TSH 400,000/=, MADINI YA TANZANITE AMBAYO THAMANI YAKE BADO HAIJAJULIKANA NA KISHA KUCHUKUA HATI YA NYUMBA NA KUTOKOMEA MAENEO YA LEMARA BWAWA LA MAJI MACHAFU.

KUFUATIA TAARIFA JUU YA TUKIO HILO, ASKARI WA JESHI LA POLISI WALIOKUWA DORIA MAENEO JIRANI WALIKWENDA KATIKA ENEO HILO KWA AJILI YA UCHUNGUZI NA KUFANIKIWA KUPATA MAGANDA MAWILI YA RISASI. JESHI LA POLISI MKOANI HAPA LINAENDELEA KUFANYA UPELELEZI PAMOJA NA KUMTAFUTA MTUHUMIWA. 

MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI CHA HOSPITALI YA MOUNT MERU KWA AJILI YA UCHUNGUZI WA DAKTARI NA MAJERUHI AMELAZWA KATIKA HOSPITALI HIYO AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HUKU HALI YAKE IKIENDELEA VIZURI.

ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.

IMETOLEWA NA KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,
MRAKIBU MWANDAMIZI WA POLISI,
(SSP) ZUBERI MWOMBEJI
TAREHE 10/04/2013.