Friday, December 28, 2012

Daraja la Huna, Marangu

Mkazi wa Sembeti, Kata ya Marangu katika Wilaya ya Vunjo Mkoani Kilimanjaro akiangalia eneo la ujenzi wa daraja la mto Huna ambalo ni zaidi ya miaka 8 sasa ujenzi wake haujakamilika huku Wananchi wa eneo hilo wakiendelea kuteseka na usafiri wa uhakika hasa wa magari katika kipindi cha Mvua. Wananchi wa eneo hilo wanamwomba Mbunge wao Augustino Lyatonga Mrema kuingilia katika ujenzi huo ambao unadaiwa kutokamilika baada ya fedha za mradi huo kutafunwa na wajanja. (picha: Father Kidevu blog)

No comments: