Wednesday, December 26, 2012

Mhe Lowassa katika Krismas Zanzibar

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa na mkewe Mama Regina Lowassa wakiwa na Wakristo wengine kwenye ibada ya Sikukuu ya Krismas iliyofanyika jana kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Mwanakwerekwe Zanzibar
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa akitoa salaam za Xmas kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mwanakwerekwe Zanzibar mara baada ya ibada ya Sikukuu hiyo jana. Mh. Lowassa yuko visiwani humo kwa mapumziko ya sikukuu hiyo, ambapo amewataka watanzania kusherehekea sikukuu hizi za krismas na mwaka mpya kwa amani na upendo huku tukilinda umoja na mshikamano uliojengwa na waasisi wetu Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume

No comments: