Tuesday, January 29, 2013

Kinana akagua ujenzi wa daraja la Malagarasi na kuhutubia wananchi wa Nguruka mkoani Kigoma

Meneja mradi wa ujenzi daraja la Malagarasi wa Kampuni ya Korea ya Hanil, Jung Sik You, (wapili kushoto) akiwatembeza Kinana (watatu kushoto), Migiro (wanne) na Nape (wa pili kulia) kwenye mradi wa ujenzi wa dajara la Malagarasi wilayani Uvinza mkoani Januari 28, 2013. Daraja hilo linatarajiwa kukamilika miezi mitatu ijayo.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kushoto) akipata maelezo ya ujenzi wa daraja la Malagarasi kutoka kwa Meneja mradi wa ujenzi daraja hilo wa Kampuni ya Korea ya Hanil, Jung Sik You.
Kinana akizungumza na mwananchi wa Kigoma Amani Mahmoud wakati akikagua ujenzi wa daraja la Malagarasi. kushoto ni Meneja mradi wa ujenzi daraja la Malagarasi wa Kampuni ya Korea ya Hanil, Jung You.
Nape akishiriki kupiga ngoma ya kuongoza matembezi kuingia mji mdogo wa Nguruka. Pembeni yake ni Asha Baraka. Matembezi hayo yaliongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
Wananchi hususan kina mama wakishangilia msafara wa Kinana upoingia Nguruka
Dokii akitumbuiza kwenye mkutano wa CCM uliofanyika Nguruka, Januari 28, 2013 ambao ulihutubiwa na Kinana
Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela akihutubia mkutano huo
Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Nguruka

Shukran: Bashir Nkoromo 

No comments: