Saturday, February 16, 2013

Dar leo: Dk Bilal asimamia zoezi la uteketezwaji wa silaha haramu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ameongoza zoezi la uteketezaji silaha haramu na kuwataka wananchi kushirikiana na serikali katika kuwafichua wanaomiliki silaha hizo mapema kabla athari haijawa kubwa zaidi. Akizungumza katika zoezi hilo la kuteketeza silaha haramu, ambalo limefanyika pamoja kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye viwanja vya Magereza, Ukonga Jijini Dar es salaam Dkt. Bilal alisema kila mwananchi ni mlinzi wa kwanza wa amani ya nchi yake na wanaomiliki silaha haramu ni wazi kuwa siyo raia wenye malengo mema na amani ya nchi zao.

Naomba kuchukua nafasi hii kuushukuru uongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kufanikisha zoezi hili ambalo linalenga kutukumbusha kuwa ili tuwe na Jumuiya bora yenye kupiga hatua, hatuna budi kuhakikisha eneo letu linabaki kuwa salama na kwamba wananchi wetu wanapata nafasi ya kufanya kazi zao za kujiongezea kipato bila kuwa na hofu ya usalama wa maisha yao. Tusipowadhibiti majangili mapema, siku wanyama wakipungua watahamia katika sekta nyingine. Kazi hii itakuwa rahisi kama tukiifanya kama Jumuiya na sio nchi moja moja. 

Asante kwa blog ya Muhidin Sufiani

No comments: