Sunday, February 3, 2013

Mwenyekiti wa CCM aongoza matembezi ya mshikamano kutimiza miaka 36 ya kuzaliwa CCM mkoani Kigoma leo

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimsalimia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana baada ya kuwasili eneo la Mnarani mjini Kigoma tayari kwa matembezi hayo. Wa pili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula na wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro
Mwenyekiti wa CCM Rais Janakaya Kikwete akiongoza matembezi ya maadhimisho ya miaka 36 ya CCM, leo asubuhi kutoka eneo la Mnarani hadi ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma leo. Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kaborou, Mama Salma Kikwete, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia)
Matembezi hayo yakipita eneo la Burega, Barabara ya Kigoma-Ujiji
"NDUGU WANANCHI, NAWAPONGEZA KWA KUSHIRIKI KWA WINGI KWENYE MATEMBEZI HAYA. HAPA SISEMI MENGI TUKUTANE MCHANA PALE UWANJA WA LAKE TANGANYIKA" Akasema Rais Kikwete wakati akizungumza na wananchi baada ya matembezi hayo. 

Asante kwa BASHIR NKOROMO

No comments: