Friday, February 8, 2013

Wakuu wa Jumuiya ya OIC wamaliza Kikao jijini Cairo

Wakuu wa nchi za Jumuiya nchi za Kiislam(OIC) wakiwa katika picha ya pamoja, mara baada ya kumalizika kwa kikao chao jijini Cairo, Alhamisi, Febr 7, 2013

Jumuiya ya nchi za Kiislamu Duniani (OIC) imezitaka pande mbili zinazopigana nchini Syria (Upande wa serikali na waasi wa FSA) kumaliza mapigano kwa njia ya majadiliano. Tangu kuanza kwa mapigano hayo mwezi machi 2011,zaidi ya watu 60,000 wameripotiwa kuuawa. Serikali ya Syria iliyo chini ya Rais Bashar Al Assad imekuwa ikizilaumu nchi za Magharibi na washirika wao wa Saudi Arabia, Qatar na Uturuki kwa kuwapa waasi silaha na fedha.

No comments: