Sunday, March 31, 2013

Picha ya mtuhumiwa wa mauaji ya Padri Mushi wa Zanzibar


Aliyekuwa mgombea wa uwakilishi jimbo la Rahaleo kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Omar Mussa Makame (37) atafikishwa mahakamani Aprili 2, mwaka huu kwa tuhuma za kumuua Padri Everistius Mushi wa Kanisa la Romani Katoliki Visiwani Zanzibar.
Mwanasiasa huyo alikamatwa na maafisa wa upelelezi, kufuatia taarifa za siri na baadae kutambuliwa mara mbili katika gwaride maalum ambalo liliwahusisha watu walioshuhudia mauaji hayo Februari 17, mwaka huu visiwani humu.

Picha kwa msaada wa zatara wa jamiiforums

No comments: