Friday, May 10, 2013

Syria ipo tayari kujibu mapigo ya Israel

Syria imetishia kujibu mashambulio yoyote mapya kutoka Israel huku washirika wake wanamgambo wa Hezbolla wakisema Syria itawapa silaha zitakazobadili kile walichokitaja kuwa silaha za kubadilisha hali ya mambo.

Naibu waziri wa mambo ya nje Faisal Muqdad amesema maagizo yametolewa ya kukabiliana mara moja na shambulio lolote jipya kutoka Israel. 

Duru kadhaa za Israel zimesema mashambulio ya Ijumma na Jumapili wiki iliyopita yalilenga shehena ya silaha zilizokuwa zikipelekwa kwa kundi la Hezbollah la nchini Lebanon lakini Muqdad amekanusha madai hayo. 

Syria Kerry na Lavrov wazungumzia Syria Syria imeukaribisha mpango wa pamoja wa Marekani na Urusi wa kutafuta suluhisho la kisiasa ili kumaliza vita vya miaka miwili lakini wakati huo huo imeshutumu sharti la Marekani la kumtaka Rais Bashar al Assad kujiuzulu. 

Assad yuko tayari kwa wachunguzi 
Serikali ya rais Assad imesema pia iko tayari kupokea kundi la Umoja wa Mataifa kuchunguza madai ya kutumika kwa silaha za kemikali nchini humo. 

Na mjini Beirut,kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah amesema Syria italipa kundi lake silaha alizozitaja kuwa zitakazobadili mkondo wa mambo yalivyo sasa na kukabiliana na Israel kutoka eneo la milima la Golan. 

Israel ilinyakua eneo hilo la Golan kutoka kwa Syria katika vita vilivyodumu kwa siku sita mwaka 1967. Israel imekuwa ikionya mara kwa mara kuwa itaingilia kati kuzuia kupewa kwa wanamgambo wa Hezbollah silaha. Hezbollah inashirikiana na majeshi ya Assad katika maeneo kadhaa nchini Syria.

Utawala wa Assad unategemea pakubwa usaidizi wa wanamgambo hao na gazeti moja la Lebanon Al Akhbar limemnukuu Assad akisema kuwa Syria italipa kundi hilo chochote kwa uaminifu wake. 

No comments: