Saturday, June 15, 2013

Bomu lalipuka katika mkutano wa Chadema Arusha

Watu wawili wanahofiwa kupoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu lililolipuka kwenye mkutano wa CHADEMA katika eneo la Soweto, kata ya Kaloleni jijini Arusha, wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi wa madiwani katika maeneo ya jiji hilo. 

Waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospitali za Seliani na Mount Meru ambapo baadhi ya watu wamejitolea vyombo binafsi vya usafiri na wengine wanashirikiana na Madaktari na Wauguzi wa hospitali hizo kutoa huduma ya kwanza. 

Kamanda wa polisi mkoani humo, Liberatus Sabas yupo katika moja ya hospitali hizo. Bomu hilo linaelezwa kuwa lilipuka kwenye mkusanyiko wa watu meta chache kutoka jukwa kuu, mwendo wa saa kumi na mbili kasoro robo jioni wakati mkutano huo ulipokuwa umekwisha na shughuli ya kukusanya michango ikiendelea. 

Viongozi wa juu wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Godbless Lema walikuwepo na wameendelea kuwepo kwenye eneo hilo. 

Watu wenye hasira wanaripotiwa kuyashambulia na kulipasua kioo gari la kutoa huduma ya kwanza (ambulance) la hopitali ya Mt. Meru lenye namba STK 8493, kwa kuwa lilichelewa kufika kuwaokoa majeruhi.  

Source: http://www.wavuti.com

No comments: