Wednesday, June 5, 2013

Majeshi Syria yadhibiti mji wa Qusair

Kituo cha televisheni cha Serikali ya Syria kinasema kuwa majeshi ya serikali yamethibiti mji wa Qusayr baada ya makabiliano makali kati yao na waasi nchini humo.

Taarifa za mapema leo kutoka mji wa Qusair zinasema kuwa kumekuwa na makabiliano makali usiku kucha ambapo runinga ya taifa la Syria imekuwa ikionyesha majengo yaliobomolewa, mbali na barabara zisizo na watu.

katika maeneo mengine, moshi mkubwa umeonekana kutanda hewani. 

Ripoti kutoka kwa wapiganaji wanaopinga serikali zinasema kuwa wameamua kuondoka katika mji huo. 

Kwa sasa mji huo ambao unadaiwa kumiliki barabara muhimu, umekuwa mahame kufuatia vita vikali vilivyochukuwa takriban majuma matatu kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa upinzani. 

Tayari maelfu ya wapiganaji wa kundi la hezbollah kutoka lebanon wameungana na vikosi vya serikali ili kuthibiti mji huo. Hatua hii inajiri wakati ambapo wajumbe kutoka umoja wa mataifa ,marekani na Urusi wanakutana mjini Geneva, Switzerland ili kujaribu kuzileta mezani pande zinazozozana.

Waasi wanasema kuwa walikuwa wameondoka kutoka vijijini eneo la Kaskazini. Televisheni ya serikali ilisema kuwa wanajeshi wa serikali na wale wa kundi la Hezbollah, waliweza kuvamia mji. 

Picha zilizopeperushwa kwenye televisheni zinaonyeshwa zilionyesha mji wa Qusair ukiwa hauna watu. Taarifa zinasema hatua ya kuuteka mji huo ni hatua nzuri kwa serikali kuuteka mji huo ulio karibu na mpaka wa Lebanon.

No comments: