Basi pekee linalofanya safari kati ya Kigoma na Mkoa wa Katavi kutoka katika kampuni ya Adventure Connection likiwa limenasa katika tope kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha. Hapa ni katika eneo la Mishamo mkoani Katavi
IDDY ALLUTE
HABARI, PICHA NA MATANGAZO.....(MAWASILIANO 0766 489048)
Sunday, March 16, 2014
Tuesday, September 3, 2013
Sherehe za ufunguzi wa ofisi ya TAKUKURU wilaya ya Kasulu zilivyofana
Muonekano wa jengo la kisasa kabisa la Ofisi za TAKUKURU wilaya ya KasuluMkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dk Edward Hoseah akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za TAKUKURU kwa ajili ya ufunguziDk Hoseah akikata utepe katika kufungua jengo hili
Picha ya pamoja kati ya Mkurugenzi Mkuu Dk Hoseah(katikati) na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya KasuluSasa umekuwa chifu wa kabila la wahaKaimu Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Kasulu Bw Onesmo Mdegera akisoma risala mbele ya mgeni rasmiWasanii wa kikundi cha KOTAG cha wilayani Kasulu wakitumbuiza wakati wa sherehe hizo
Wednesday, August 28, 2013
Radio Imaan FM na Kwa Neema FM zarudi hewani
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUREJESHWA KWA URUSHAJI MATANGAZO RADIO IMAAN FM NA KWA NEEMA FM RADIO
1.0 Utangulizi:
Mnamo tarehe 26/02/2013 Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilitoa uamuzi wa kuvifungia vituo vya utangazaji vya Radio Imaan ya mjini Morogoro na Kwa Neema FM Radio ya jijini Mwanza baada ya kukiuka Sheria na Kanuni za Utangazaji.
Kamati ya Maudhui iliuita uongozi wa vituo hivyo tarehe 11/02/2013 na tarehe 14/02/2013 ili kujitetea na vyote vilikiri kosa. Baada ya kutafakari utetezi wa Radio Imaan na Radio ya Kwa Neema FM na kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Utangazaji, Kamati iliamua kutoa adhabu kwa vituo vyote viliwi kama ifuatavyo:-
a) Vituo vyote vilipewa onyo pamoja na kufungiwa kurusha matangazo kwa kipindi cha miezi sita kuanzia tarehe 26/02/2013;
b) Vituo vyote vilitakiwa kuithibitishia Mamlaka ya Mawasiliano na Kamati ya Maudhui kwa maandishi kuwa hawatarejea kutenda kosa la aina hiyo au linalofanana na hilo. Ikiwa vitarudia Kamati ya Maudhui haitasita kuvifutia leseni zao za utangazaji.
2.0 Kutekeleza adhabu na hatua zilizochukuliwa na vituo hivyo na Mamlaka ya Mawasiliano:
Baada ya Uamuzi huo kusomwa, vituo vyote viwili vilianza kutekeleza adhabu mara moja kama ilivyotakiwa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utangazaji. Mamlaka ya Mawasiliano ilipokea barua ya udhibitisho wa kutofanya kosa tena yaani “Commitment letter” pamoja na sera ya uhariri (Editorial Policy) na ratiba ya vipindi kutoka kwa vituo vyote viwili.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilifanya ukaguzi kwa vituo vyote viwili ili kujiridhisha na kuzipitia sera za uhariri pamoja na mwongozo wa vipindi kabla ya kuvifungulia.
3.0 Kurejeshwa kwa Matangazo
Kamati ya Maudhui iliandika barua tarehe 27/08/2013 kuhusu kuvifungulia vituo hivyo vya utangazaji vya Radio Imaan ya mjini Morogoro na Kwa Neema FM Radio ya jijini Mwanza baada ya kutumikia adhabu kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utangazaji. Vituo hivi vimeanza kurusha matangazo yake kuanzia leo tarehe 28/08/2013 baada ya muda wa adhabu kuisha.
Kamati ya Maudhui inapenda kutumia fursa hii kuvionya vyombo vya habari vya utangazaji vya redio na televisheni kuwa makini katika kutekeleza masharti ya leseni pamoja na kufuata Sheria na Kanuni za Utangazaji. Kamati ya Maudhui haitasita kutoa adhabu kali au kuvifungia vituo vitakavyokiuka Masharti ya leseni, Sheria pamoja na Kanuni za Utangazaji au hata kuvifutia leseni zao.
Kamati ya Maudhui inatoa wito kwa vyombo vya habari vya utangazaji kuzingatia Sheria, Kanuni na Masharti ya leseni ilikuboresha Sekta ya Utangazaji na kudumisha amani nchini.
Eng. Margaret Munyagi
Mwenyekiti,
Kamati ya Maudhui Ya TCRA,
S.L.P. 474,
DAR ES SALAAM.
28/08/2013
----
KUHUSU KAMATI YA MAUDHUI:
1.1. Kamati ya Maudhui ni kamati iliyoundwa kwa mujibu wa sehemu ya IV kifungu cha 26 (1) cha Sheria Namba 12 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003, na marekebisho yake katika kifungu 173 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) Mwaka 2010
Kwa mujibu wa sheria, majukumu na kazi za Kamati ya Maudhui ni pamoja na:-
(a) Kumshauri Waziri wa Sekta kuhusiana na Sera ya Utangazaji nchini;
(b) Kushughulikia malalamiko kutoka kwa watangazaji na watumiaji wa huduma za utangazaji nchini;
(c) Kusimamia na kuhakikisha kuwa kanuni za utangazaji zinafuatwa.
(d) Kusimamia na kufuatilia maudhui ya vituo vya utangazaji.
1.2. Kamati hii ilianza kazi zake Oktoba 2012 baada ya kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (MB) tarehe 4 Desemba, 2012.
1.3. Kamati ya Maudhui inaundwa na wajumbe watano. Wanne ni wateuliwa wa Waziri mwenye dhamana ya Sekta ya Utangazaji na Mwenyekiti ambaye huchaguliwa miongoni mwa wajumbe wa Bodi ya TCRA. Muundo huo umetolewa na sehemu ya 26 (2) ya Sheria ya TCRA ya Mwaka 2003.
Majina ya wajumbe ni kama ifuatavyo:-
i. Mhandisi Margareth Munyagi -Mwenyekiti
ii. Bwana Walter Bgoya -Makamu Mwenyekiti
iii. Bwana Abdul Ngarawa -Mjumbe
iv. Bwana Joseph Mapunda -Mjumbe
v. Bwana Yusuf Nzowa -Mjumbe

Thursday, August 8, 2013
Thursday, August 1, 2013
Monday, July 29, 2013
Wednesday, July 17, 2013
Mbio za mwenge zilivyofana mkoani Kigoma, 2013
TAKUKURU walishiriki kwa kuonesha kazi zao na kutoa elimu kwa hadhira iliyohudhuria Jeshi la Polisi nalo lilitoa elimu kupitia mkakati wa Polisi Jamii na Utii wa Sheria bila Shuruti. Pia dawati la Jinsia la Jeshi hilo pia lilikuwepoMkuu wa wilaya ya Kigoma Ramadhani Maneno (mwenye tracksuit) katika picha ya pamoja na wakimbiza mwenge KitaifaUjirani mwema: Kikundi cha burudani kutoka Burundi kilinogesha mbio hizo za mwengeSoko katika kijiji cha Bitale ni moja ya miradi iliyozinduliwa na mwenge mwaka huu
Tuesday, July 16, 2013
Monday, July 15, 2013
Breaking News: Majambazi yateka Biharamulo
Habari zilizoifikia blog hii hivi punde zinaeleza kuwa majambazi yapatayo manane yakiwa na bunduki aina ya SMG yameteka magari katika pori la Kasindaga lililopo wilayani Biharamulo.
Mabasi yaliyotekwa ni NBS, RS na Mohamed Trans yaliyokuwa yakielekea Dar na Arusha.
Aidha vitu mbalimbali vimeporwa vikiwemo Simu na fedha taslimu.
Saturday, July 13, 2013
Usafiri wa treni umerejea
Baada ya kukwama kwa siku tatu katika stesheni ya Kigoma, hatimaye usafiri wa treni kuelekea Dar umerejea kama inavyoonekana.
Subscribe to:
Posts (Atom)