Wednesday, October 10, 2012

Lowasa awataka warembo Miss Tanzania kutumia Urembo kujitengenezea ajira



WAZIRI Mkuu Mstaafu wa Tanzania, na Mbunge wa Monduli, Edward Lowasa amewataka warembo wanaoshiriki mashindano ya urembo ya Redds Miss Tanzania 2012 kutumia nafasi hiyo waliyopata kutengeneza ajira kwao na vijana wenzao. Lowasa ameyasema leo wakati warembo wanaowania taji hilo walipomtembelea nyumbani kwake eneo la Ngarash mjini Monduli na kuzungumza nao juu ya mambo mbalimbali ya kisiasa, uchumi, utalii na sanaa ya urembo. “ninyi ni vijana, mnanguvu na hakika mkiyatumia vyema mashindano haya kwa malemngo yanayostahili mnaweza kufika mbali kimaisha kwa kuwa wabunifu wa vitu mbalimbali vya kufanya katika jamii na kujipatia ajira yenu binafsi na hata kuajiri watu wengine,”alisema Lowasa. Lowasa ambaye amekuwa mstari wa mbele nchini katika kuhakiskisha vijana wengi wanapata ajira nchini amesema sanaa ya urembo ikitumika vyema inamanufaa katika jamii na ikitumiwa vibaya italeta matatizo na kuonekana sio kitu cha muhimu. Akitolea mfano wa Washindi wa Taji la Miss Tanzania waliopita hasa Hoyce Temu ambaye ni Miss Tanzania 1999 kwa jinsi alivyo kuwa mbunifu na kipindi chake cha Mimi na Tanzania ambacho mbali na kutoa fursa ya kuweza kuibua matukio na maisha ya hali tofauti ya Watanzania lakini pia ametoa ajira kwa wote anaofanya nao kazi. Akizungumzia juu ya ziara hiyo ya warembo hao ya kutembelea Vivutio vya Utalii nchini hasa katuka Mikoa ya Kanda ya Kaskazini amesema kuwa ni jambo jema hasa kuziangatia kuwa utangazaji wa vivutio vya utalii vya nchi yetu upo chini hivyo warembo watasaidia jamii kuelewa na kujenga utamaduni wa kuitembelea vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani. Kuhusiana na hali ya kisiasa nchini Lowasa amewaambia warembo hao kuwa Tanzania ipo katika hali nzuri ya kisiasa jambo ambalo linazidi kuchochea maendelea na kuleta umoja wa kitaifa ambao unawawezesha watu kuishi kwa amani. “Siasa yetu ni safi na kiukweli Serikali ya CCM inazidi kuidumisha hali ya amani nchini jambo ambalo linawezesha hata ninyi kutembea bila matatizo kutoka sehemu moja hadi nyingine, alisema Lowasa. Pia Lowasa aliipongeza Kamati ya Miss Tanzania chini ya Mkurugenzi wakew Hashim Lundenga kwa kazi kubwa ya kuandaa mashindano hayo makubwa nchini ambayo yamekuwa yalityoa ajira mbalimbali kwa washiriki wake na fursa za elimu. Warembo wanaowania taji la Redds Miss Tanzania wapo katika ziara ya kutembelea vivutio vya utalii Kanda ya Kaskazini pamoja na kufanya shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na kuchangia watoto yatima na waishio katika mazingira magumu. Kesho Oktoba 11, watatembelea Hifanyi ya Bonde la Ngorongoro na kujionea maajabu mbalimbali yaliyopo katika eneo hilo.
 

No comments: