Monday, October 22, 2012

Mtoto wa Gaddafi auwawa katiaka uwanja wa mapammbano

Hayati Muammar Gaddafi
Khamis Gaddafi 28 mtoto wa kiume wa mwisho wa Colonel Gaddafi inasemekana ameuwawa katika uwanja wa vita kati ya majeshi ya serikali ya Libya na yale ambayo bado yanamuunga mkono aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Col Gaddafi katika mji wa Bani Walid. Msemaji wa serikali ya Libya,Libya National Congress Omar Hamdan alisema Khamis alifia vitani baaa ya mapambano makali lakini hakufafanua zaidi.

Kama ilivyokuwa baada ya kifo cha babake mwaka mmoja uliopita na mwili wa Khamis unapelekwa Misrata mji wa tatu kwa ukubwa Libya. Khamis alichukua mafunzo yake ya kijeshi huko Urusi na baadae akaja kuunda kikosi cha Brigade ya 32 mahsusi kwa ajili ya ulinzi wa babake, kikosi hicho kilituhumiwa kwa kuendesha mateso ubakaji na mauaji.

No comments: