Sunday, December 23, 2012

Katiba mpya yapita Misri

Katiba mpya ya Misri iliyoandikwa na bunge linalodhibitiwa na Waislamu imepitishwa kwa asilimia 64 katika duru ya pili ya kura ya maoni. Afisa mmoja wa chama cha Udugu wa kiislamu amefahamisha kuwa katiba mpya ya Misri imepitishwa na wapiga kura wa nchi hiyo baada ya kufanyika duru ya pili ya kura ya maoni. 

Afisa huyo ameyakariri matokeo ya kura ambayo siyo rasmi ya chama chake. Katika duru ya pili ya kupiga kura iliyofanyika hapo jana watu wa Misri waliipitisha katiba mpya kwa asilimia 64. Katika duru ya kwanza asilimia 57 ya washiriki walipiga kura ya ndio. 
dw

No comments: