Monday, December 10, 2012

Siku ya Maadili mkoani Kigoma na wilaya ya Kibondo

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mwananchi katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji wameadhimisha siku ya Maadili kwa kupanda miti katika eneo la shule yao. Jumla ya miti 50 ya kivuli na matunda imepandwa

HUKO KIBONDO NAKO, MAMBO YALIKUWA HIVI
Kaimu kamanda wa TAKUKURU Kibondo-Godwin Kahensa
Mmoja wa makamanda akitoa msaada wa Sabuni kwa mgonjwa


Mmoja wa makamanda wa TAKUKURU bw. Nelson akifanya utambulisho
Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Ofisi ya Kibondo Mkoani Kigoma imewataka Watumishi wa Idara za Serikali na asasi za Binafsi kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na viapo vya kazi zao.

Kaimu kamanda wa Taasisi hiyo Dk. Godwin Kahensa amesema hayo wakati akizungumza na uongozi wa Hospitali ya wilaya hiyo katika maadhimisho ya siku ya Haki za binadamu na maadili iliyofanyika leo.

Dk.Kahensa amesema, ikiwa watumishi watafanya kazi kwa kuzingatia maadili jamii itapata huduma bora.

Aidha,katika maadhimisho ya siku hiyo ambayo duniani kote inaadhimishwa kila disemba 9 ya kila mwaka,Dk Kahesa amesema siku hiyo hapa Nchini inaadhimishwa Disemba 10 kwa kuwa Disemba 9 ni siku ya Uhuru. 

 Asante(picha za Kibondo) kwa ngarakwetu blog 

No comments: