Monday, December 24, 2012

TAKUKURU yathibitisha Afisa wake kuuawa

DAR ES SALAAM, Tanzania 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imethibitisha kuwa kwamba mtumishi wa taasisi hiyo, Bhoke Ryoba ameuawa kwa kupigwa risasi jana usiku. 

"Tumekuwa tukipokea simu nyingi kutoka kwa watu mbalimbali wakihitaji kufahamu ukweli kuhusu tukio la kupigwa risasi kwa Mtumishi wa TAKUKURU - Bhoke Ryoba. Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dk. Edward Hoseah, anapenda kutoa ufafanuzi kuhusu tukio hili kwamba ni kweli Mtumishi Bhoke Ryoba amefariki dunia jana usiku - Jumamosi tarehe 22/12/2012 baada ya kupigwa risasi" Imesema taarifa iliyotolewaleo na makao makuu ya TAKUKURU. 

Taarifa hiyo imesema, Uchunguzi wa Polisi kuhusu chanzo cha tukio hilo bado unaendelea.

No comments: