Saturday, January 12, 2013

Ajali mbaya yatokea Posta jijini Dar

Baadhi ya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakimshusha mwenzao baada ya kujigonga kwenye mti na kujeruhiwa vibaya na kupasuka sehemu za kichwani wakati akiwa kwenye Lori lenye namba za usajili 5514 JW 07 aina ya IVECO kandokando ya barabara ya Samora jirani na Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam jioni hii.

Majeruhi akiingizwa katika Bajaji tayari kwa ajili ya kupelekwa hospitali
Lori aina ya IVECO ambalo majeruhi huyo alikuwa amepanda huku likiwa limesheheni mzigo mkubwa .
Hii ndio Barabara ya Samora ilipotokea ajali hiyo.
Hapa ndipo alipojigonga majeruhi na kupasuka sehemu za kichwani (Picha na Habari Mseto Blog)

No comments: