Tuesday, January 8, 2013

Mhe Lowassa asaidia VICOBA jimboni kwake

Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Edward Lowassa (MB) amevipatia vukundi saba vya Vikoba vilivyopo Wilayani Monduli, kiasi cha shilingi milioni nane kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao. Lowassa amesema yeye ni mkereketwa mkubwa wa Vikoba huku akisisitiza kuwa ni chachu ya maendeleo na kumkwamua mtanzania kutoka katika umasikini. Kila kikundi kimepata shilingi millioni moja ambapo kikundi kilichofanya vizuri kimeongezewa shilingi millioni moja zaidi. Pichani ni Mh. Lowassa akipeana mkono na mwenyekiti wa Vikoba Kijiji cha Monduli Juu, Dawson Kaaya wakati viongozi wa vikundi hivyo walipomtembelea nyumbani kwake Monduli.
Baadhi ya wanavikoba wa Monduli Mjini wakimsikiliza Mh. Lowassa
Mmoja wa viongozi wa vikundi vya vikoba Kijiji cha Monduli Mjini akisoma risala
Mhe Edward Lowassa akipewa zawadi na Bi Arafa Ismail kutoka katika vikundi vya Vikoba Monduli mjini ambao walikwenda kumtembelea nyumbani kwake. Kushoto kwa Mhe ni Bw. Dawson Kaaya ambaye ni Mwenyekiti wa Vikoba Monduli Mjini

No comments: