Friday, January 4, 2013

Usafiri wa Treni kwenda Bara wasitishwa

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawataarifu abiria wote na wananchi kwa jumla kuwa kutokana na kuharibika njia ya reli eneo la Stesheni ya Mikese jana usiku, safari ya treni ya abiria ya kutoka Dar es Salaam kwenda Bara iliyopangwa kuondoka leo Ijumaa Januari 04, 2013 saa 8:30 mchana haitakuwepo.

Taarifa ya siku ya kuondoka itatangazwa baadae kulingana na ushauri wa Jopo la Wataalamu wa TRL waliopelekwa kusimamia ukarabati wa eneo hilo . Tafadhali atakayesoma taarifa hii amuarifu mwenzake. Uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza

     IMETOLEWA NA AFISI YA UHUSIANO KWA 
      NIABA YA MKURUGENZI MTENDAJI-TRL 
       MHANDISI KIPALLO AMAN KISAMFU
       DAR ES SALAAM, JANUARI 04, 2013

No comments: