Friday, January 4, 2013

Breaking News: BOTI yazama Ziwa Tanganyika

Habari zilizotufikia punde zinaeleza kuwa, Boti iliyokuwa inasafiri kutoka Kusini mwa ziwa Tanganyika kuelekea nchi jirani ya Burundi imezama jirani na kijiji cha Herembe katika kata ya Sigunga wilayani Kigoma. Boti hiyo ilikuwa imebeba abiria na mizigo. Hadi tunawaletea taarifa hii, jumla ya miili yaa watu wanane(08) ilikuwa tayari imeshaopolewa na jitihada zaidi zinaendelea kutafuta miili mingine. Mpaka sasa haijulikani idadi ya watu waliokuwemo ndani ya boti hiyo.

No comments: