Friday, March 29, 2013

Taarifa ya Polisi: Mtuhumiwa wa mauaji ya Padre Mushi akamatwa

MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI
KAMISHINA WA POLISI ZANZIBAR

MAKAO  MAKUU YA POLISI ZANZIBAR

29.03.2013
Ndugu waandishi wa habari,

Assallam Aleykum

Najua leo ni siku ya mapumziko na siku ya ibada kwa waumini wote. Leo tupo katika Ijumaa Kuu lakini pia ni siku ya sala ya pamoja kwa Waislam katika misikiti mbalimbali. Nimeamua tukutane leo kwa sababu tatu. Kwanzza kwa kuendelea kudumisha doria za mjini na vijijini kwa kutumia gari, Askari wa migu, pikipiki na mbwa ili kuhakikisha usalama unadumu Visiwani hapa. Tunaendelea kutoa ushauri wa kiusalama na kushirikiana kwa karibu zaidi na wananchi wote kuona maisha na mali zao zinakuwa salama. Tunawaomba wenye mahoteli ya kitalii na nyumba za starehe kuwa karibuna jeshi lao la Polisi  pamoja na kufuata ushauri wote wa kiusalama wanaopewa kila wakati.

Pili tumeitana hapa kutoa shukurani kwa wananchi wote. Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi wote kwa ujumla wao kwa ushirikiano mkubwa mnaotupa. Si rahisi kutaja kila msaada tunaopata kutoka makundi mbalimbali ya wananchi wteu, lakini tukiri msaada tunaopata ni mkubwa na umetusaidia na unaendelea kutusaidia katika kudumisha amani na utulivu. Hata hivyo, napenda kutoa shukurani zangu za dhanti kwa nyinyi waandhishi wa habari hasa wa ahapa Zanzibar kwa kuwa karibu na ofisi yang na kuchangia kwa kiwango kikubwa mchakato mzima wa kudumisha amani Visiwani hapa.

Jambo la tatu tuliloitania hapa ni kupeana taarifa juu ya maendelea ya kesi ya mauaji ya Padri Evarest Mushi. Najua si nyinyi tu waandishi wa habari lakini Watanzania wote wanatka kujua maendeleo ya upelelezi wa tukio hili. Jeshi la Polisi liliwaahidi litawajulisha kila hatua iliyofikiwa juu ya upelelezi wa shauri hili. Mpaka hapa tunapozungumza upelelezi wa shauri hili umefikia pahala pazuri na jalada la shauri hili limeshapalekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka kwa hatua za kisheria. Muhusika wa mauaji haya tayari amekamatwa na ametambuliwa na watu walioshuhudia tukio hilo. Mtakumbuka Jeshi la Polisi mbali na hatua kadhaa za kiupelelezi walizozichukua ilikuwa ni pamoja na kuchora michoro ya sura ya mtu kwa kutumia  watu walioshuhudia tukio hilo. Baada ya kuitoa picha hiyo katika vyombo vya habari mablimbali vya kiulinzi, w3ananchi, vyombo vya habari na mitandao ya kijamii muhalifu hyo ametambulika na kutambuliwa.

Jeshi la Polisi liliahidi kutoa milioni kumi kwa watu watakaosaidia kupatikana kwa muhalifu huyo. Ahadi ile ipo pale pale na mwananchi aliyesaidia kutoa utambuzi Jeshi la Polisi litamzawadia kiwango hicho cha fedha, laini kwa usalama wa shahidi huyo na kwa sababu za kiupelelezi tukio la kumkabidhi fedha hizo hatutaliweka bayana katika vyombo vya habari.

Jeshi la Polisi linaendelea kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kufanikisha upelelezi wa matukio mengine yaliyopita. Tunawaahidi kuendelea kuwasisitiza na kutotoa siri wala kuwataja wale wote wanaotupa taarifa za kihalifu.

Mwisho kabisa, naomba niwashukuru tena wananchi wote wa Zanzibara kwa kuwa karibu na ofisi yangu na Jeshi la Polisi kwa ujumla katika mapambano ya vitendo vya kihalifu.

Ahsanteni.

Ijumaa karimu.

MUSSA A. MUSSA - CP
KAMISHNA WA POLISI
ZANZIBAR

No comments: