Monday, January 21, 2013

Lowassa, Mtemvu wahani msiba wa Sufiani Kusaga, mumewe Khadija Kusaga

Mhe. Lowassa akimpa pole mfiwa, Mama Khadija Kusaga wakati alipofika nyumbani kwake Keko Maghorofani jijini Dar es salaam jana.
Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mhe. Edward Lowassa na Mbunge wa sasa wa Temeke, Abbas Mtemvu, jana Jumapili jioni walikuwa ni miongoni mwa waombolezaji waliofika kuuaga mwili wa Marehemu Sufiani Bakari Kusaga, huko nyumbani kwake Keko Maghorofani jijini Dar es salaam. Marehemu Kusaga alikuwa ni mume wa Mbunge wa zamani wa Jimbo la Temeke ambaye sasa hivi ni Katibu wa CCM-Kishapu, Mh. Khadija Kusaga. 

Source: http://www.wavuti.com

No comments: