Monday, January 21, 2013

Ukuta waangukia magari stendi ya Ubungo

Asubuhi ya leo imetokea ajali kwenye kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam,baada ya ukuta wa eneo la maegesho ya magari kuangukia magari zaidi ya ishirini yaliyokuwa yamegeshwa katika eneo hilo.

Watu wanne wamejeruhiwa na kupelekwa hospitali. Hakuna mtu aliyeripotiwa kupoteza uhai. Chanzo cha ajali chaelezwa ni kitendo cha mkandarasi kubomoa ukuta huo bila kuutahadharisha umma.

No comments: